Wote Scheme

Mafao yanayotolewa  kama yafuatayo:

 a) MAFAO YA UZEENI

 Sifa Zinazohitajika

         i) Hutolewa kwa mwanachama alifikisha umri wa kustaafu wa kuanzia miaka 55 au zaidi kama itakavyo amriwa na bodi ya wadhamini kwa vipindi tofauti.

         ii) Kupata Mafao ya Uzeeni mwanachama awe amechangia katika Mfuko kwa kipindi kisichopungua miaka 15 (miezi 180)

 Taratibu za Utoaji wa Mafao

        i) Pensheni itakayolipwa katika mtirriko wa malipo kwa kipindi maalum itakokotolewa kutokana na mapato yatokanayo na uwekezeja wa michango ya mwanachama.

 Nyaraka zinazohitajika

       i) Fomu ya maombi ya mafao iliyojazwa na mwanachama

       ii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa au uthibitisho wa miaka ya mwanachama

       iii) Maelezo ya Banki- Jina na akaunti kwa ajili ya kulipa Mafao ya kila mwezi

Zingatio: Mwanachama yeyote atakae amua kujitoa kwenye Mfumo atalipwa michango yake pamoja na riba. Endapo mwanachama atafariki, wategemezi wa mwanachama anaweza kuleta maombi ya malipo ya mafao kwa niaba ya mwanchama aliyefariki.

 

b) MAFAO YA AFYA

 Sifa Zinazohitajika

       i) Mwanachama atakuwa na sifa ya kupata fao la baada ya kuchangia kwenye Mfuko kiasi kisichopungua Tsh. 60,000.00

      ii) Mwanachama atapata bima ya afya sawasawa na wanachama wngine wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

 

Taratibu za Utoaji wa Mafao  ya Afya

       i) PPF itawalipia gharama za mwaka kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wanachama wote wenye sifa.

      ii) Mwanachama atapatiwa kadi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kupata huduma za kiafya kwenye hosptitali zilizoainishwa.

 Nyaraka zinazohitajika

       i) Fomu za NHIF zilizojazwa kikamlifu

       ii) Picha moja paspoti yenye kivulinyuma cha rangi ya bluu

c) MKOPO wa ELIMU

 Sifa Zinazohitajika

Mwanachama atapata mkopo wa elimu baada ya kuchangia katika Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita.

 Taratibu za Utoaji Mkopo wa Elimu

      i) Mkopo wa Elimu hutolewa kwa mwanachama husika au mtoto wa mwanachama.

     ii) Marejesho ya mkopo huu yatafanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja au katika kipindi kisichozidi miaka mitano (5).

 

Nyaraka zinazohitajika

     i) Kitambulisho cha uanachama wa PPF

     ii) Udhibitisho wa taarifa za michango ya mwanachama kutoka PPF

 Zingatio: Pamoja na nyaraka zilizotajwa  hapo juu, mwanchama atajaza na kuwasilisha kwenye Benki fomu ya maombi ya mkopo wa elimu ambayo atapatiwa kutoka banki.

 

d) MKOPO WA MAENDELEO

Sifa Zinazohitajika

      i) Sifa za mkopo, mwanachama lazima awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita

 Taratibu za Utoaji Mkopo wa Maendeleo

      i) Mkopo utatolewa kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu.

      ii) Marejesho ya mkopo ni kati ya mwaka mmoja hadi mitano (5).

     iii) Kiasi cha mkopo ambacho mwanachama awazeza kukopeshwa kitaamuliwa na Bank kwa mashauliano  na Mfuko.

Nyaraka zinazohitajika

     i) Kitambulisho cha uanachama wa PPF

     ii) Udhibitisho wa taarifa za michango ya mwanachama kutoka PPF

Zingatio: Pamoja na nyaraka zilizotajwa  ya hapo juu, mwanchama atajaza na kuwasilisha kwenye Benki fomu ya maombi ya mkopo wa maendeleo ambayo atapatiwa kutoka banki.