Uwekezaji

Uwekezaji wa michango ya wanachama ni moja kati ya kazi kuu nne za Mfuko.

a) Nyaraka zinazosimamia shughuli za uwekezaji

 • Sera ya Mfuko ya Uwekezaji inayotolewa na  Bodi ya Wadhamini
 • Miongozo ya uwekezaji, inayotolewa na Benki Kuu na Mdhibiti wa Hifadhi ya Jamii ( SSRA)
 • Sera ya Mfuko ya Uwekezeji wa Muda Mfupi inayotolewa na Bodi ya Wadhamini
 • Sera za Mfuko za Kifedha zinazotolewa na  Bodi ya wadhamini

 b) Falsafa ya Uwekezaji

Falsafa ya uwekezaji inundwa na nguzo zifuatazo:

 • Uhifadhi wa mtaji, ukuzaji na uendelezaji
 • Kinga dhidi ya mfumko wa bei (faida ya uwekezeji ni lazima iwe zaidi ya mfumko wa bei)
 • Kuhakikisha kunakuwepo na ukwasi wa kutosha kutekeleza mahitaji ya sasa.
 • Kuwa na uwiano katika maeneo uwekezaji ambapo  Mfuko umewekeza ili kuepuka majanga
 • Mapato yanayotokana na uwekezaji mbadala

 c) Maeneo ya Uwekezaji

Ukomo wa Uwekezaji kwa kuzingatia asilimia ya mali za Mfuko ni kama hapo chini

 • Hati fungani za Serikali- 20%-70%
 • Mikopo kwa serikali ya moja kwa moja 10%
 • Hati fungani kwa makampuni binafsi -20%
 • Mali isiyohamishika – Majengo ya ofisi, starehe, shule pamoja na nyumba za kuishi 30%
 • Hisa – uwekezaji katika kumiliki hisa katika makampuni binafsi na ya umma – 20%
 • Uwekezaji wa pamoja kwa Mifuko  30%
 • Mikopo kwa taasis binafsi na vyama vya ushirika 10%
 • Miundombinu - 25%
 • Amana katika Benki za bashara- 35%