Fao la Uzazi

Sifa Zinazohitajika

 i) Hutolewa kwa mwanachama mwanamke

 ii) Mwanachama anatakiwa awe amechangia kwa kipingi kisichopungua miaka 2 (miezi 24) na

iii) Awe amechangia kwa kipindi cha mwaka 1 (miezi 12) mfululizo kabla ya kujifungua

iv) Dai liwasilishwe ndani ya siku 90 tangu kujifungua

 

Taratibu za Utoaji wa Mafao ya Uzazi

 i) Mafao ya mkupuo ya fedha taslimu hulipwa kwa mwanachama anayejifungua mtoto kila baada ya miaka mitatu

ii) Mafao yatalipwa kwa kila uzazi na si kwa idadi ya watoto wanozaliwa

iii) Malipo haya yatalipwa hadi mara 4 kila baada ya miaka 3 mara tu mama anapojifungua.

iv) Inapotokea mtoto amepoteza maisha ndani ya miezi 12 tokea kuzaliwa kwake, mwanachama ataweza kupata mafao yake bila ya kusubiri hadi miaka 3 ipite.

 

Nyaraka zinazohitajika katika katika kukokotoa Mafao ya Uzazi

 i) Fomu ya maombi ya mafao iliyojazwa na mwajiri kwa usahihi.

ii) Barua Uthibitisho wa kujifungua kwako kutoka kwa mwajiri

iii)  Barua/nakala ya kadi ya kliniki kutoka katika hospitali iliyosajiliwa ambako mwanachama alihudhulia cliniki.

iv) Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto