Benefit: Maternity Benefit

Mafao ya Uzazi 

Mwanachama lazima awe mwanamke mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 

Hutolewa kwa mwanachama mwanamke aliyejifungua mtoto/watoto kila baada ya miaka 3

Mwanachama awe amechangia kwa kipindi cha mwaka 1 (miezi 12) mfululizo kabla ya kujifungua

Mwanachama awe amechangia kwa kipindi kisichopungua miaka 2 (miezi 24) na linatolewa ndani ya siku 90

 

Mpango wa malipo:

Mwanachama atalipwa kiasi cha Tsh 1,000,000 mara baada ya kujifungua salama

Malipo haya yatalipwa hadi mara 4 kila baada ya miaka 3 mara tu mama anapojifungua.

Inapotokea mtoto amepoteza maisha ndani ya miezi 12 tokea kuzaliwa kwake, mwanachama ataweza kupata mafao yake bila ya kusubiri hadi miaka 3 ipite.

Fomu zinazohitajika:

Fomu ya madai ya PPF iliyojazwa kwa usahihi

Barua iliyothibithishwa na mwajiri wako kutoka kwa hospitali ambayo mwanachama anapata huduma za cliniki

Nakala ya cheti kilichothibishwa cha kuzaliwa kwa mtoto (yaani Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto)


(Updated on 2015-08-26)