Kuhusu PPF

PPF – Kuanzishwa

PPF ni Mfuko wa Pensheni ulioanzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF [Sura Na. 372, Marejeo ya Mwaka 2015] kwa wanachama wote kutoka sekta rasmi na zisizo rasmi za kiuchumi

Mfuko huu ulianzishwa July, 1978.

 

Mabadiliko ya Jina na Chapa

Sheria ya Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (yaani The Social Security Regulatory Authority Act) ya Na. 8 ya 2008, ilipelekea kufanyika kwa mabadiliko kwenye jina letu la zamani lililokuwa likijulikana kama ‘’Mfuko wa Pensheni wa Mashirikia ya Umma’’ na kuwa ‘’Mfuko wa Pensheni wa PPF’’ ili kuweza kutanua wigo wa uandikishaji wanachama.

Aidha, chapa yetu mpya inaonyesha kiwango cha ushindani na mabadiliko yaliyopo sokoni na dhamira yetu ya kutimiza ahadi kwa kutoa mafao yanayozingatia ubunifu na utumiaji wa teknolojia sambamba na utoaji huduma kwa wateja zenye viwango vya kimataifa kutoka kwenye timu yenye uzoefu wa kutosha inayotumia teknolojia ya kisasa zaidi.

 

DIRA

Kuwa Mfuko wa kuigwa katika utoaji wa huduma za Hifadhi ya Jamii

 DHIMA

Kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine ya hifadhi ya jamii kwa kutumia wafanyakazi wenye weledi wa kutosha na teknolojia ya kisasa kwa ufanisi na wakati

 

Maadili Yetu

Mfuko utatimiza dhima yake na kukuza utamaduni uliojiwekea ambao unaamini katika: huruma, weledi na kufanya kazi kwa pamoja na kwa bidii

Majukumu makuu ya Mfuko ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa wanachama wake

Uendeshaji wa Mfuko

Mfuko una Mifumo mitatu ambayo ni Mfumo wa Asili wa Pensheni, Mfumo wa Uwekezaji Amana, Mfumo wa 'Wote Scheme'